Mechi Za Kirafiki O.F.A Wiki Iliyopita

Jana Jumapili Tarehe 8/9/2013 Vijana Wa Kituo Cha Orange Football Academy (OFA) U-16 NA U-19 Wamecheza Mechi Za Kirafiki Na Matokeo Ni Kama Ifuatavyo:-
Vijana Wa OFA U-16 SAA 8:00pm Wamecheza Na Timu Ya Barcelona Matokeo OFA 4 - 3 Barcelona, Magoli Ya Ofa Yamefungwa Na, Jaffar Ussi (Kipindi Cha Kwanza, Abdulkarim (D Jong) Kipindi Cha Kwanza, Abdulhalim Mabrouk (Kizizu) Kipindi Cha Pili Na Adam Ali (Edo) Kipindi Cha Pili.

Ofa Iliweza Kuwatumia Vijana Wapya Ambao Walitokea Katika Bonanza La Ofa. Huku Kaka Zao Wa U-19 Saa 10:30pm Wakicheza Na Shangani Na Matokeo Ofa 1 - 1 Shangani, Goli La Ofa Limewekwa Kimiyani Na Hilali Said (Boha) Kipindi Cha Pili.

Kituo Cha Ofa Baada Ya Kumalizika Mfungo Wa Mwezi Wa Ramadhani Na Skukuu Ya Idd, Kimeanza Rasmi Maandalizi Yake Ya Kijiweka Fiti Na Kuwatayarisha Vijana Wa U-19 Kwa Misingi Bora, Kupitia Kamati Ya Central Kuanza Na Kuendelea Na Zoezi La Upitishaji Na Uhakiki Wa Wachezaji Wote,

Kituo Cha Ofa Kimefurahishwa Na Zoezi Hilo Na Kimefanikiwa Kukamilisha Kwa Vijana Wa Kituo Cha Ofa Kuhakikisha Wanapitisha Na Uhakiki Kwa Upande Wetu Unakamilika Kwa Vizuri.

Kwa Upande Wa U16 Kituo Kimeweza Kupata Vijana Wenye Vipaji Kupitia Bonanza Letu La Kutafuta Vipaji Kwa Vijana Wa Mitaani Na Kupata Vipaji Kutoka Timu Tofauti Kwa Kuwajumuisha Katika Kituo Chetu.

Mategemeo Yetu Kituo Safari Hii Kitatoa Vijana Kwenda Timu Tofauti Kubwa Za Ndani Na Nje Ya Nchi.