Mechi Ya Kirafiki U16

ORANGE FOOTBALL ACADEMY (OFA)  JUMAMOSI 14/9/2013 KIMECHEZA MECHI YA KIRAFIKI U-16 NA TIMU YA SAP SOAP KATIKA KIWANJA CHA MAO NA MATOKEO ORANGE 1 - 0 SAP SOAP, GOLI LA OFA LIMEFUNGWA NA ADAM ALI (EDO) DAKIKA YA 56.

Orange Football Academy yatoa kichapo cha Goli 1 - 0 dhidi ya timu ya Sap Soap kutoka kwa Mchina mwanzo katika mchezo safi wa kirafiki uliochezwa Mao B , Goli la vijana wa OFA limefungwa na Mchezjai Adam Ali (Edo) kipindi cha pili ch amchezo dakika ya 56. hata hivyo vijana wa ofa walipoteza nafasi nyingi za wazi..

Vile vile Vijana wa OFA U-19 watacheza mechi ya kirafiki na timu ya New Vission katika Kiwanja cha Mao tse tung.

Kituo cha kukuza na kuendeleza vipaji vya soka  kwa vijana cha OFA kinatoa pongezi kwa vijana wa Copa Coca Cola kutoka Mkoa wa Mjini Magharibi kwa ushindi mzuri walioupata na kushinda Taji la mashindano hayo kwa vijana wa Umri chini ya miaka 15.