UKARABATI UWANJE WA AMAAN

 
Wakati harakati za ukarabati za uzekaji nyasi bandia katika uwanja wa Amaan Zanzibar ukiendelea uwanja ambao hutumiwa kwa vilabu vikubwa katika mechi zao mbalimbali za ligi pamoja na timu ya Taifa pamoja na mashindano mengine mengi ya kitaifa na kimataifa suala ni je?  kwanini uwanja huo unafanyiwa umuhimu wa ukarabati huku viongozi wakuu wa michezo wakijua kwamba lengo ni kuufanya uwanja huo kutumika katika future kwa lengo la kulinufaisha taifa katika michezo mbalimbali?
 
suala ni je? uwanja huo unajengwa kwa nguvu zote kwaajili ya maendeleo ya taifa la baadae au taifa lililopita?je uwanja huo unajengwa kwa lengo la akina Mzee Mwinyi:Abdul Majham na akina Shioni Mzee na wengineo  watakuja kuliwakilisha taifa kama miaka ya nyuma au lengo ni kwa vijana wachanga wanaochipukia kuja kuliwakilisha taifa?
 
Pichani uwanja wa Amaan ukiwa katika matengenezo huku picha njingine vijana chipukizi wakijichezea soka katika majaa bila ua wahusika kujali au kuona kuwa nguvu zao za ujenzi wa uwanja wa Amaan hawa vijana ndio wachewaji wa uwanja huo kama tunavyoona kila mwaka na pia kama tulivyoona vijana wa U15  wa wilaya ya mjini magharibi kutwaa ubingwa wa copa cola cola Tanzania.
Pichani Vijana wa Zanzibar wakiwa wanacheza mpira jitihada inatakiwa kuchukuliwa na mamlaka husika kuweza kuwaendeleza vijana hawa kwani hio ni hazina kubwa kwa Taifa suala ni kwanini wizara ya michezo inashindwa kutenga maeneo kwa kila jimbo kwaajili ya vijana kama hawa maeneo ambayo yatakuwa ni viwanda vya kuibua vipaji vya wachezaji kwa vilabu mbalimbali kufatilia kujipatia vipaji katika maeneo hayo ambapo kama inavyojulikana soka ni ajira ya vijana wengi duniani kote kama ambavyo inapewa kipaumbele katika nchi za Brasil na nchi zote zilizoendelea katika ulimwengu wa soka. 
Kutokana na mpaka sasa kutokuwa na mradi wowote wa kuwatengea vijana maeneo yao kwa kila jimbo nchini basi hata Jitihada inashindikanwa  zichukuliwa mamlaka zinazohusika japo  kukinusuru kiwanja kama hiki na jaa hili ili kutoa nafasi kwa watoto hawa kucheza michezo mbali mbali kama walivyokutwa na mpiga picha hii wakicheza mpira na jaa hilo likiingia kwa kasi kwenye kiwanja hicho cha Mao.
 
Je hata kutenga eneo la wananchi wa maeneo haya kutupa taka zao na hawa chipukizi kujitafutia ajira kupitia soka tunahitajia msaada au fikra kutoka kwa wazungu? kweli mamlaka husika inashindwa hata mifuko 10 ya saruji kuifunga hio sehemu ngodo ya ukuta iliyobomoka na kunusuru utupaji taka holela ambao baada ya vijana hao kujitafutia vipaji vyao na kujiepusha na matendo maovu na pengine kujipatia ajira zao kutokana na vipaji vyao mwisho wao ni kujipatia maradhi mbalimbali yatokanayo na uchafu huo katika maeneo hao.
kama Taifa linawekeza viwanja kwaajili ya wachewaji wa baadae; na wachewaji wenyewe wa baadae wanachewa katika majaa; hivyo nguvu zote na muda wa kuwekeza utakuwa ni bure; kwani wachewaji tunaowatayarishia hivyo viwanja matokeo yake inabidi tusubiri Rubbish Players na Rubbish game kwani hili itakuwa ndio tulilopanda na tutarajie mavuno hayo hayo; huwezi kupanda muhogo ukavuna kiazi.
Je hata hili linahitaji Wazungu?