NYOTA WA COCA COLA CUP WALINDWE KWA KILA HALI

Pichani mabingwa wa coca cola cup wakipata chakula cha mchana walichoandaliwa na mwenyekiti wa wilaya wilaya ya mjini magharibi ndg Hassan Haji na baadae kufuatia kikao maalum cha kuwapongeza nyota hao wadogo kwa kazi waliyoifanya ya kutwaa ubingwa wa soka wa mashindano nchini.
 
kwa niaba ya Kituo Cha kukuza vipaji vya soka nchini Oranje Football Academy kinatoa pongezi kwa chipukizi hao uongozi mzima uliowaongoza nyota hao kutwaa ubingwa huo,uongozi wa wilaya ya mjini Magharibi pamoja na wadau wote waliotoa michango yao na wale waliopeleka hisia zao kufatilia michuano hio kwa vijana kutokana na ushirikiano wao huo ndio ulioleta matunda hayo katika mkoa huo wa mjini magharibi.
 
Kwa niaba ya uongozi mzima wa O.F.A unawaomba wachezaji ,viongozi na wadau wote wakiwemo waheshimiwa wa baraza la uwakilishi pamoja na wabunge waktika mikoa mingine Zanzibar kuiga mfano na kufata njia za wadogo zao wa wilaya ya mjini magharibi ili na wao mwakani waweze kuiwakilisha mikoa hio na kuleta maendeleo makubwa ya soka Zanzibar.
 
Wakati huohuo baadhi ya wadau wa soka wanaoishi nje wametoa mawazo yao kwa uongozi wa wilaya ya mjini magharibi hasa ule wa cnetral league "KUANZISHA SHERIA YA KUWALINDA NYOTA HAO" pamoja na nyota wengine ambao wana uwezo mkubwa kisoka katika mechi zao mbalimbali za mashindano au kirafiki ili kwenda sambamba na nyota wa ulaya.
 
Lengo ni waamuzi kuwalinda vijana hao katika mechi zao ili kuepuka kuapata majeraha yanayoweza kusababisha kumalizika kwa uwezo wao huku wakiwa na umri mdogo kwani kutokuwalinda nyota hao kunasababisha baadhi ya wachezaji wengine wazembe kukusudia kwa makusudi kabisa kuwaumiza au kuwavinja kabisa vijana wenzao eti tu ni kutokana na uwezo huo wa kusakata soka.
 
waliongeza kufanya hivyo kutaweza kutoa nafasi nyota hao kutoogopa sana viwanjani na hivyo kuwaruhusu "kufanya vitu vyao " ambapo itawaongezea uwezo zaidi kitu ambacho kitalisaidia sana taifa katika mfumo huo ambao ni wa miaka mingi barani ulaya kuwalinda nyota wao hata kama wapo katika madaraja ya chini.
 
Mwisho wadau hao wameelezea matumani yao kuona serikali itawalinda nyota hao na kuelekeza matumani yao kuwa wanatarajia kuwaona nyita hao katika kikosi cha taifa chini ya umri wa miaka 16 mwakani na chini ya umri wa miaka 17 msimu mmoja baada kabla ya nyota hao kuwa katika timu ya taifa kubwa baada ya miaka mitatu tu ijayo.