MAZOEZI YAENDELEA VIZURI O.F.A

Chipukizi wa Orange Football Academy wanaendelea vizuri na mazoezi katika viwanja vya nje vya  Mao Tse Tung katika kujitayarisha na ligi itakayoanza hivi karibuni.
 
Wakiwa na baadhi ya nyota wapya katika vikosi vyao  vyote na kujiimarisha katika lengo lake la kuibua vijana wenye uwezo mkubwa kisoka ili kulisaidia taifa kuondokana na "ukame" wa vipaji ukilinganisha na mataifa mengine ya Afrika yalivyopiga hatua katika kuimarisha mpango huo kwa vijana katika mataifa yao.

Kituo cha  kuibua,kukuza na kuendeleza vipaji vya soka kwa vijana nchini O.F.A safari hii imeongeza nguvu mpya kupitia katika BONANZA iliyoianzisha mwezi wa Ramadhani na kuibua vipaji vipya kadhaa kutoka vijana wa mitaani ambapo nyota hao kwa mara ya kwanza wataweza kuonekana viwanjani wakifanya vitu vikubwa ambavyo vilikuwa vimefichikana mitaani kutokana na vilabu,na wahusika wakuu wa michezo nchini  kutokuwa na mipango wa kuibua vipaji kama hivyo vikubwa  mitaani kwa lengo la kulisaidia taifa letu.