RATIBA YA UJIO WA KOCHA MFARANSA O.F.A

 

Hii hapa ni ratiba fupi ya ujio wa kocha kutoka nchini Ufaransa kupitia kwa Partners wetu wa Afrisoccer Consulting Ltd,

Kituo chetu cha kukuza na kuendeleza vipaji vya soka nchini kikiwa na malengo ya kuzalisha vipaji bora nchini kwa maendeleo ya taifa letu kinapenda kutoa ratiba hii rasmi ya ujio wa mwalimu huyo ambae ataweza kuleta maendeleo katika kituo chetu cha O.F.A, tunawaomba wadau wote ndani na nje ya nchi kukisaidia kituo chetu hicho kwakuwa ndio kituo kinachoongoza kwa sasa nchini kutembelewa na wataalamu mbalimbali kutoka nje kwa malengo ya kuibua vipaji kwaajili ya taifa letu,
tunawaomba wadau wote popote walipo kutoa mchango wowote utakaoweza kuleta manufaa na maendeleo katika kituo chetu ili kufikia malengo yake na kuikomboa nchi yetu katika soka kwani soka pia mbali ya kuwa ni ajira kwa vijana,biashara kwa wawekezaji,pia ni balozi mzuri wa nchi nje ya mipaka yetu na duniani kote pamoja na kuwajenga vijana katika mzingira mazuri kiafya vile kuwaepusha vijana hao na matendo maovu.

Tunawaomba wadau wengine wanamichezo wengine na makocha  kujitokeza kwa wingi  katika mazoezi kama hayo kila yanapotokea kwaajili ya kujipatia pia mbinu za kisoka kutoka kwa wataalamu hao wanaokuja katika kituo cha O.F.A ili yaweze kuwasaidia pia katika kukuza vipaji nchini.

 

 ORANGE OFA PROGRAM