TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

 Kituo cha kukuza soka kwa vijana nchini cha Oranje Football Academy kinapenda kukutaarifu kwamba siku ya tarehe 27/10/2013 Jumapili tutapokea ugeni kutoka Kampuni ya Afrisoccer ukiambatana na Kocha Mfaransa Mr. Patrick Liewing aliewahi kuwa kocha wa timu ya Simba Sports Club ya Dar es Salaam. Kampuni ya Afrisoccer Consulting LTD inahusika na masuala ya “Scouting, Management, Consultancy and Capacity Building in Football” ambayo ni mshirika wa kituo cha Orange Football Academy (O.F.A).

 

Kituo cha  (O.F.A) kupitia timu yake ya Oranje Football Academy (O.F.A) siku hiyo ya Jumapili tarehe 27/10/2013 saa 3:00 asubuhi kitafanya mazoezi ya pamoja katika kiwanja chake cha mazoezi MAO kwa vijana wa U – 17 na U – 19 na  kuonyesha vipaji vyao wakati huo kocha wa zamani wa timu ya Simba Sports Club ya Dar es Salaam Mfaransa Mr. Patrick Liewing na Maafisa wa Kampuni ya Afrisoccer wakiwa kiwanjani hapo kuangalia vipaji vya wachezaji.

Vijana wa kituo cha Orange (O.F.A) siku hiyo hiyo ya Jumapili tarehe 27/10/2013 wakati wa saa 7:30 za mchana watacheza mechi ya kirafiki na timu ya Shangani F.C kwa lengo la kuangali vipaji na kuona uwezo wa vijana wa kituo chetu na kuangalia jinsi gani kituo kinalea na kuzalisha vipaji hivyo na kuhakikisha tunapiga hatua mbele zaidi kwa vijana wetu, na kupelekea vijana hao kupata timu za kucheza soka la kulipwa ndani na nje ya nchi kwa lengo la kuwa wachezaji wa kulipwa na kukipatia tija na sifa kituo cha (O.F.A).

 

Wakati huo huo kocha Mfaransa Mr. Patrick Liewing na maafisa wa Kampuni ya Afrisoccer kutoka Dar es Salaam watapata nafasi ya kuangalia uwezekano wa kuchukua vipaji vitakavyojitokeza katika mazoezi na mchezo wa mechi ya kirafiki kwa lengo la kuwatafutia timu kujiendeleza nje ya nchi.

 

Naambatanisha na Ratiba kamili ya shughuli husika.

 

Ahsante,

Hashim Ali Ahmada

Katibu Timu ya Orange Football Academy (O.F.A).

P.O. Box 1596, Fax +255 2231791

Tel: +255 777433520 / 412150, Tel: +255 024 2231833

www.//oranjefootballacademy.blogspot.com 

www.ofaznz.net

 

 

Taarifa