COACH PATRICK LIEWING AVUMBUA VIPAJI VIKALI O.F.A

Katika tukio la tarehe 27/10/2013 la ujio wa Kocha Mfaransa Mr. Patrick Liewing akiambatana na Maafisa wa Kampuni ya Afrisoccer ambao ni Partnership wakuu wa timu ya Kituo cha kukuza vipaji vya soka kwa vijana nchini Orange Football Academy (O.F.A).
Baadhi ya wachezaji (vijana) wa kituo ambao walimvutia zaidi kocha huyo Mfaransa ambae alitaka kituo kiwatunze na kuhakikisha kinawalinda kwa lengo la kuwapatia faida pamoja na kituo pia.
 
vijana wenyewe ni:
1. Adam Ali Issa (Edo) (U - 16) - ambae ana uwezo wa kucheza position yoyote akiwa kiwanjani pia ni mfungaji mahiri katika   baadhi ya mechi  alizocheza, katika mechi 7 ana magoli 5.
 
2. Saleh Salum Saleh (Wabu) (U - 16) - ambae anacheza nafasi ya Midfield. 
 
3. Abdulrahman Shaaban Sulubu (Jerad) (U - 16) - ambae anacheza nafasi ya Midfield.
 
4. Hilal Said Abdalla (U - 19) - ambae ana uwezo wa kucheza position yoyote akiwa kiwanjani zaidi Defender.
 
5. Hamed Mohammed Nassor (U - 19) - ambae ana uwezo wa kucheza position tofauti kiwanjani zaidi kiungo mshambuliaji.
 
6. Ali Majid Ramadhan (U - 19) - ambae ana uwezo wa kucheza nafasi ya ushambuliaji ambae alionyesha uwezo mkubwa na anaumbo zuri la kucheza nafasi ya ushambuliaji, 
katika mazoezi na mechi ya majaribio iliyochezwa wakati wa mchana alifunga goli safi.
 
7. Ferej Salum Khamis (U - 19) - ambae ana uwezo wa kucheza nafasi ya winga Midfield.
 
Na katika mchezo wa kirafiki uliochezwa kati ya kituo cha Orange (O.F.A) na timu ya Shangani wakati wa mchana baada ya vijana wa O.F.A kufanya mazoezi mazito na kutakiwa mchana wake kucheza mechi ili kuangalia uimara wa vijana hao, vijana wa Orange (O.F.A) walitoka sare ya goli 1 - 1 dhidi ya timu ya Shangani f.c.
 
Tunaomba wadau kukisaidia kituo chetu kwa vifaa vya mazoezi,vifaa vya shule na baadhi ya mahitajio madogo madogo ili tuweze kulisaidia taifa letu kupitia katika kituo chetu kutoa ajira nyingi iwezekana kwa vijana wa kituo chetu pamoja na maendeleo ya taifa letu.