UFUNGUZI WA CENTRAL LEAGUE

Pichani Mgeni rasmi naibu katibu mkuu uvccm ndugu Shaka Hamdu Shaka akimkabidhi akimkabidhi ngao ya hisani nahodha wa timu ya Mwembebeni United baada ya kushinda kwenye mchezo huo dhidi ya timu ya Arizona mchezo huo ulikuwa maalum wa ufunguzi wa mashindano ya Central 

 
kocha mkuu wa timu ya Taifa Salum Bausi akishuhudia mchezo huo na kuangalia uwezekano wa kuibua vipaji kwaajili ya timu ya Taifa ya Zanzibar kama alivyofanya kocha wa zamani wa timu hio Stewart Hall ambae sasa ni kocha wa Azam f.c alipomuibua Seif Abdalla "karihe" kutoka Orange Football Academy moja kwa moja kujiunga na timu ya Taifa ya Zanzibar Heroes.
 

Tunauhakika katika daraja la Central League kuna vipaji vikubwa kulinganisha au kupita kaka zao wa Primier League hivyo ni vizuri kwa kocha Bausi sio tu kuangalia ufunguzi wa mashindano hayo,bali kufatilia (yeye na benchi lake) mashindano hayo na kuibua vipaji vilevile kutoa changamoto kwa vijana hao na kuwa na matumaini mazuri ya kujiunga na timu hio ya Taifa kutokana na uwezo huo kisoka.