KOCHA YA TIMU YA TAIFA YA ITALIA ATUA ZANZIBAR

Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar Said Ali Mbarouk, akizungumza na Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Italia, Cesare Prandelli, alipowasili Zanzibar, Akizungumzia juu ya kuazisha kwa Ushirikiano wa masuala ya michezo na Utalii, wakiwa katika chumba cha VIP Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, wakifuatilia mazungumzohayoKocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Zanzibar Salum Bausi na Rais wa ZFA Ravia Idarous Faina.
 
Tunawaomba wahusika wakuu wa michezo nchini kumpatia nafasi kocha mkuu huyo wa Italia nafasi ya kuwaona vijana wetu wa Academy za nchini ili kuangalia maendeleo ya vijana kutoa makosa na mchango wake wa maendeleo ya vijana nchini kwa manufaa ya taifa letu,ikiwezekana apatiwe nafasi ya kuona mechi ya/za soka za vijana hao ili kupata maoni yake na ikiwezekana kuwa balozi wa soka la vijana nchini huko nje.
Tunatarajia ujio wa kocha huyo sio tu utainufaisha timu kubwa ya Taifa ya Zanzibar bali pia itakuwa ni mwanzo wa maendeleo kwa timu za vijana nchini ambazo kwa muda mrefu zimekuwa zikiachiliwa wenyewe tu kujiendeleza bila ya kupatiwa wataalamu wa soka kama hao.
 
picha kwa hisani ya Zanzinews.