O.F.A U20 NA U17 ZASHINDA MICHEZO YA LIGI

Chipukizi wa kituo cha Orange football Academy wameanza  vyema  Ligi ya Vijana kwa timu za kituo cha hicho  kushinda mechi zake za Round No.1 
Kwa ngazi ya Central U - 20 na Junior U - 17.
 
OFA U-20    1-0  F.C LEOPARDS
Goli la OFA limefunga na Ali Mohammed Ali (bamba)
 

OFA U-17    2-1  F.C ROYAL 

Magoli ya OFA yamefunga na Adam Ali (Edo) dakika ya 25 na Abdulrahman Shaaban  (Gerad) dakika ya 63.
 
Akiongea na Website hii inayomilikiwa na kituo cha Onranje Football Academy kocha mkuu Hashim Ahmada alisema vijana wamechaza vizuri michezo yote miwili na kushinda lakini ligi ndio kwanza imeanza hivyo watazidi kuimarika kadri ligi itakavyoingia kasi katika michezo inayofata, 
alimalizia kwa kusema vijana wanaendelea vizuri na mazoezi kujianda na mechi zifatazo mwishoni mwa wiki hii.