LIEWIG KUTUA O.F.A HIVI KARIBUNI

Wakati Stewart Hall ambaye amesaini kuifundisha akademi mpya ya Sunderland ya Kidongo Chekundu na ile ya Elit Football Academy ya jijini Dar es salaam.

 

naye Patrick Liewing aliyekuwa Simba na hapo nyuma akiwa ni mmoja wa viongozi wa banchi la ufundi la makocha wa Paris Saint Germain ya Ufaransa, Asec Mimosa ya Ivory Coast, alikuwa katika banchi la ufundi la timu ya Taifa ya Egypt pamoja na kufundisha timu nyingi kubwa za West Afrika yeye ametia saini kufanya kazi kwa pamoja na  akademi zinayosimaiwa na Afrisoccer Consulting Limited ya Dar es salaam  ambapo moja ya academy hizo ni Orange Football Academy ya Zanzibar,

Kocha Patrick Liewig alitarajiwa kutua  nchini Desemba Mosi kuanza kazi kwenye Academy hizo ikiwemo Orange Football Academy ya Zanzibar katika mpango mpya wa "Football Clinic-Training" mfumo mpya wa kuibua vipaji nchini na kutafutia nafasi ya kusakata soka nchini kama Ufaransa,Sweden na nyinginezo barani ulaya.

 

kocha Liewig tayari kwa kushirikiana na Afrisoccer Consulting Limited ya jijini Dar es salaam amefanikiwa kupata kampuni nchini Ufaransa ya kufanya kazi "partnership" pamoja na Afrisoccer ambao pia ni "partner wa O.F.A, jina la kampuni hio tayari tunalo "kapuni" tunasubiri wasemaji wakuu wa suala hili wa Afrisoccer kuliweka uwanjani na kulitambulisha rasmi kwa vyombo vya habari nchini.

Katika mpango huo wa "Football Clinic" Kocha mfaransa Liewig ambae awali alikuwa atue nchini december mosi sasa anatarajiwa kutua mwishoni mwa mwezi huu wa November na atakuwepo nchini kwa muda wa siku 15 badala ya 10 za mpango wa mwanzo ambapo atakuweko Dar es salaam na Zanzibar katika Orange Football Academy, 
"Nimeongeza muda  zaidi ili kuweza  kuibua vipaji vingi zaidi  iwezekavyo ili  nipate nafasi zaidi kuanza kuviwekea malengo vipaji hivyo" alisema kocha Liewig ambae chanzo chake kipo katika oranje football academy.

 

hayo ni moja ya maendeleo ambayo yanatarajiwa kuanza kujitokeza nchini hivi karibuni ambapo Zanzibar itanufaika na mpango huu maalum ambao wataalam  hao watauleta hapa nchini kwa Kushirikiana na wananchi wenyewe ambao ni wewe na mimi na kila mmoja wetu ambae ana ndoto ya maendeleo nchini.

lakini tujiulize hao watu kutoka nje ambao lengo lao ni kuona vijana nchini wanapata ajira kupitia soka pamoja na kuitangaza nchi kupitia soka zaidi ni kuutangaza Zanzibar kiutalii kupitia soka je viongozi wetu wanalichukulia suala hili umuhimu gani wakati Utalii ndio zao kuu la mapato Zanzibar?

je hao wataalamu wa kuibua vipaji kutoka nje watakuwa wanafanya kazi kwa lengo la kuwapatia nafasi vijana au wananchi wa Zanzibar wakati viongozi wahusika wa nchi wao hawaoneshi mchango au kujua lolole kuhusu suala hilo?
 
kwanza matengenezo yangelianza kutengeneza na kuboresha viwanja kwa ajili ya vijana ambao ndio matunda ya baadae (CENTRAL LEAGUE).
 
mfano: kiwanja cha Mao Nje, Small Simba, Kikwajuni, Malindi, Shangani, Miembeni, Ujamaa, Black Fighter na vyenginevyo hasa ukizingatia kiwanja cha Mao Ste Tung kikitanuliwa na kutengenezwa viwanja vya nje vitapotea tutakosa kiwanja cha kuchezea mazoezi na mechi za Central League na ndicho pekee kinachokitegemea kwa mechi za Central na Wageni kutoka Dar es salaam na Pemba wanakifurahia na kukitumia vyema.
 
imefika wakati kuliona hilo, kwa kuhakikisha soka la vijana linakuwa, kwa kuwa ndio msingi wa soka letu na taifa kwa ujumla, tunaiomba Serikali kupitia ZFA, wafadhili wa ujenzi wa Mao Tse Tung kuzingatia ujenzi wao wa kiwanja hicho, kwa kuhakikisha wanajenga viwanja viwili kwa kuboresha kiwanja cha Mao Ste Tung cha Ndani na kujenga cha Mao Ste Tung cha nje kwa ajili ya Soka la vijana (Central League) na dhani ni vyema na ni busara kuliko kuangalia mbele huku nyuma tukiwa hatujafanya chochote ni makosa.
 
"kuondoka nyumbani kwako akaufunga kwa kufuli kubwa mlango wako na ukahakikisha kuwa hakuna uharibifu wowote wa uvunjaji mlango huo huku ukiwa mlango wa nyumba hujaufunga" huu ni mfano hai kwa kuona Bajeti ya Ujenzi wa kiwanja cha Amani na Kiwanja cha Mao Ste Tung ambacho kinatazamiwa mara tu baada ya kumalizika ujenzi wa Amani kitafanyia matengenezo, matengenezo ambayo yatakiathiri kiwanja chengine cha Mao nje ambacho ni rasilimali kubwa kwa soka la vijana. vile vile kwa mechi za madaraja ya vijana Central League.
 
kukikosesha usingizi kituo cha Orange Football Academy (OFA) ambacho kwa sasa ni kama wanavyosema ni "chachu" ya kuleta maendeleo ya soka kwa vijana  kwa kukosa sehemu au eneo la kufanyia mazoezi ili kukuza na kuendeleza vipaji kwa vijana hilo nadhani sio suala sahihi kwani pindi uwanja wa Mao tse tung utakapoanza utanuzi wake na kukifanyia matengenezi chipukizi hao watakosa kiwanja cha mazoezi hivyo hio mipango yote ya makocha wanaowatafuta kuwaleta nchini kipitia kwa washirika wake itaweza kushindikana kwani  mpira siku zote ni uwanja si vinginevyo.
 
Hebu tuliangalie hili kwa kina, inawezekana kujenga kiwanja kimoja na chapili kikaboreshwa na hali ikawa sawa tu.ujenzi huo unaweza ukauwa kabisa soka la vijana wasipo kuwa makini wakandarasi na ZFA pamoja na Serikali kwa jumla kwavile kiwanja hicho cha Mao tse tung B ndicho kiwanja kimoja wapo kinachotuwa na vijana wote wa mjini magharibi kuchezea mechi zao za ligi na ndicho kiwanja kilichochangia kwa hali kubwa kuibua vipaji vya wachezaji wa COPA COCA COLA ambao walitwaa ubingwa hivi karibuni wa Tanzania kwa vijana wenye umri huo, je kiwanja hicho kikiondoshwa vijana gani tena hapo tunatarajiwa kuwapata kuwaweka katika timu zetu za Taifa za watoto hapa Zanzibar?
 
Kwanini tushindwe kuvisaidia vilabu vidogo vidogo kwa kuvipatia sehemu za kufanyia mazoezi na mechi tukimbilie viwanja kuvijenga majengo mbali mbali kwa uvamizi wa nguvu za wenye nguvu na kuviharibu kwa kujengwa kiwanja kimoja cha mechi huku ukipoteza viwanja vingi kwa ajili ya mazoezi na mechi kwa soka la vijana au kuwatengenezea maeneo yao maalum ya viwanja kwaajili ya vijana hao?
 
Wahusika wa mila,utamaduni na michezo, je hii sio ndio moja ya kazi zao kwa vijana wao? na hata wale wa Utalii je Soka si Utalii? angalia nchi kama Brasil ni watalii wangapi wanaingia nchini mwao kila siku huku Soka ndio unabeba bendera ya nchi yao kama kichochezi cha watalii hao kwenda nchini humo?
 
Tunapenda kuipigia mfano Zanzibar kwa vipaji vya kuzaliwa kwa soka ni kama nchi Uholanzi ambayo ni nchi ndogo sana lakini mipango mizuri unaifanya nchi yao kila siku kuzalisha nyota wapya wanaowika barani ulaya na kuzipita nchi kubwa sana nyingi barani ulaya.
 
Kama Zanzibar kutakuwa na mpango mzuri kutokana na vipaji vyake inaweza kuwa ni soko kuu la soka katika bara la Afrika na soko kuu la Utalii katika kanda ya Afrika mashariki na kati.