CHIPUKIZI WA O.FA WAZIDI KUWA NA VIWANGO ZAIDI

Vijana wa kituo cha kukuza vipaji vya soka nchini Orange Football Academy wameonyesha matumaini zaidi katika mazoezi baada ya nyota hao kutambua umuhimu wa malengo yao kisoka ambayo ni moja ya kazi kama kazi nyinginezo zozote duniani.

 Kama kawaida kwa umri mdogo baadhi ya vijana ambao wana vipaji vikubwa kisoka lakini kutokuwa na muono mzuri kama soka ndio inaweza kuwa kazi yake hivyo kuwafanya nyota hao kutokaza buti kuendeleza vipaji vyao ila hufanya soka ni sehemu ya furaha na starehe kwao.
 
Kituo cha kukuza vipaji vya soka kwa vijana nchini Oranje Football Academy inazidi kufarijika kwa nyota hao "makinda" kujitambua na kila mmoja kutilia mkazo kwa juhusu za ziada kati yao na kila mmoja wao akiwa na ndoto za kufikia katika kiwango kikubwa na kuamini soka ndio itakayokuwa ajira yake kama ambavyo ni ajira kwa wanasoka viongozi wa soka wote duniani.
 
Wakati huohuo Kiungo mkali mchezeshaji wa U17 Abdul-Halim Mabrouk Hafidh "kizizou" amerejea mazoezini rasmi baada ya kumaliza adhabu ya mwezi mmoja na nusu aliyopewa kutokana na utovu wa nidhamu,nyota huyo mkali katika sehemu ya kiungo alikosekana katika mechi zote zinazoihusu U17 kwa muda huo aliokuwa akitumikia adhabu hio na kuomba radhi kwa uongozi pamoja na wachezaji wenzake jambo ambalo lilipata ridhaa kwa pande zote mbili na nyota huyo kurejeshwa kujumuika na wenzake kundini.
 
Kiungo huyo  Abdulhalim  Hafidh  alisema "nimerejea katika timu yangu nadhani mtanipokea na kuwa pamoja nami, mimi nipo tayari kushirikiana na wenzangu wote kupitia timu yangu hii ya kituo cha OFA".
 
Naomba mnipokee, na kusahau yaliyopita, huu ni wakati mwengine wa kufunga na kufungua ukurasa mwengine" maneno ambayo alitamka nyota huyo kwa uongozi na wachezaji wenzake na kukubalika kurejea katika klabu yake ambayo ndio pekee inayoweza kumsaidia kufikia malengo yake kwa sasa, kocha Hashim Ali Kibabu amempokea Abdulhalim (Kizizu)na kumtaka kutuliza akili yake na kujituma mazoezini kulingana kimchezo na wachezaji wengine ambao wamekuwa pamoja kwa muda wa mwezi mmoja na nusu zaidi yake  alioupoteza bila ya kuwa kundini. 
 
Jumamosi tarehe 23/11/2013 O.F.A U17 Junior League imetoka sare ya 1-1 dhidi ya Harish Mwambao, bao la O.F.A lilifungwa na Adam Ali "Edo" katika dakika ya 31 ambapo nyota huyo tayari ana mabao 2 katika mechi mbili za ligi hio.
Harash walisawazisha bao hilo katika dakika ya 73 katika mechi iliyochezwa katika kiwanja cha mao tse tung B.
 

Mechi ya no 3 itachezwa  siku ya  30/11/2013 saa  9:30 katika kiwanja cha mao tse tung O.F.A itajitupa kiwanjani dhidi ya  Mapembeani.
 

Katika mechi za awali za ligi  kituo cha Orange football Academy imeanza  vizuri  Ligi ya Vijana kwa timu zake kushinda mechi zake za Round No.1kwa ngazi ya Central U20 na Junior U17.
 
OFA U20    1-0  F.C LEOPARDS
Goli la OFA limefunga na Ali Mohammed Ali (bamba)
 
OFA U17    2-1  F.C ROYAL

Magoli ya OFA yamefunga na Adam Ali (Edo) dakika ya 25 na Abdulrahman Shaaban  (Gerad) dakika ya 63.


Katika hatua nyingine nyota wa Orange Football Academy  Seif Abdalla Karihe yupo nchini Kenya  katika kikosi cha Timu ya Taifa ya Zanzibar ambayo inashiriki kombe la Challenge, Zanzibar Heroes  imeondoka Jumapili tarehe 24/11/2013 Zanzibar kuelekea Nchini Kenya ikiwa na kikosi cha wachezaji 20.

 
Kituo cha O.F.A kipo bega kwa bega na kijana wao huyo (ambae mpaka sasa Azam f.c inatumia mabavu kumtumia nyota huyo kama mchezaji wao bila ya kumlipia ada ya malipo kama sheria za soka zinavyosema) 
Mpaka hivi sasa Oranje Football Academy inaidai Ruvu Shooting malipo ya nyota huyo ya kuchukua kituoni hapo na kumsajili bila ya kulipia ada kwa mujibu wa shereia za Zfa,Tff,Caf na Fifa, kumtumia mchezaji huyo katika ligi bila idhini ya O.F.A,
Pia inaidai Ruvu Shooting kurejesha fedha zote ilizopokea kutoka Azam F.c kwa kumuuza mchezaji huyo kama mchezaji wao ambapo fedha hizo zilitakiwa kulipwa katika kituo hicho cha O.F.A.
Kituo hicho kutokana na dharau za Azam f.c za kuzipinda sheria za soka za kumsajili kimabavu nyota huyo, kituo cha I.F.A kinaidai klabu hio fedha za malipo za mchezaji huyo kwa misimu yote anayoendelea kuitumikia klabu hio na atakayoendelea kuitumikia bila idhini na malipo kwa mujibu wa sheria za soka na "kumbatiza"kuwa mchezaji wao huku wakilijua suala hilo sambambamba na Mudathir Yahya kiuongo mwengine mkali ambapo fedha zao zingeweza kuwasaidia vijana wengine wadogo katika Academy hiyo.
 
Baada ya uongozi wa O.F.A kuwasiliana mara kadha na uongozi uliopita wa "Tenga regime" na kuamua tu kwamakusudi kuwa vipofu au viziwi kutotaka kulipatia ufumbuazi suala hilo, tunatarajia uongozi mpya wa Tff ambao unaonekana kuwa ndio utakao kuwa uongozi "bomba" katika historia ya soka nchini baada ya kuchagua kamati maalum ya kusimamia soka kwa vijana na kwa bahati nzuri ndani ya uongozi huo yupo Ally Mayay ambae ni mjumbe wake huku akiwa pia ni kiongozi wa Afrisoccer Consulting Limited ambao ni patrters wa O.F.A hivyo tunayo matuma yeye atakuwa ni mtetezi mkuu wa haki za vijana nchini kote kwavile shuhuli hii ipo katika kamati yake ya vijana.
 
kuitwa kwa "karihe"katika  timu ya Zanzibar Heroes ni faraja kubwa sana kwa O.f.a na pia kwa upande mwengine inasikitika kumuona nyota wake mwingine mudathir Yahya kuwa nje ya kikosi hicho kitu ambacho kinatokana na kuwa nje katika kikosi cha kwanza cha Azam f.c katika mashindano ya ligi kuu.
 
Kwaniaba ya kituo cha OFA kinaitakia  baraka na kila kheri  timu hiyo ya Zanzibar Heroes ambayo imesheheni vipaji kwa vijana wengi kuimarishwa kwenye kikosi hicho kufanya vizuri katika michuano hio nchini Kenya.
 
Kituo cha O.F.A kinahakikisha kuengeza juhudi zaidi za kuzalisha vipaji na kutoa Karihe wengine iwezekanavyo ambapo mipango hiyo kwa sasa imekamilika kuhakikisha kituo kinazidisha ubora katika mafunzo yake kushirikiana na Afrisoccer Consulting Limited ya Dar es salaam  ambapo hata Mfaransa Mr. Patrick Liewing kwa muda mfupi tu aliweza kuvumbua vipaji kadhaa katika kituo hicho cha O.F.A na pia alisema  kuwa juhudi zifanywe zaidi  vipaji hivyo viendelezwe na kuvilinda visiporwe na vilabu vyengine bila ya mafanikio ya kituo hicho.