ORANJE FOOTBALL ACADEMY WASHINDA TENA LIGI

Vijana wa Orange Football Academy wameendelea kufanya vizuri katika michuano ya ligi za vijana yanayoendelea baada ya ushindi kwa timu zake za U20 na U17 katika viwanja tofauti.
U20 siku ya jumamosi tarehe 07-12-2013 iliweza kuichapa bao 1-0 timu F.C Villa (mpira pesa) kwa goli lililopachikwa kimiani na chipukizi mkali wa O.F.A Yussuf Songoro katika dakika ya kwanza ya mchezo.
Habari za kusikitisha katika pambano hilo ni kuwa mfungaji wa bao hilo la O.F.A Yussuf Songoro baada ya kufunga bao hilo nyota huyo katika dakika ya 25 alitolewa nje baada ya kuumia goti na kumfanya akimbizwe hospitali ambapo alipatiwa matibu na kufungwa (P.O.P) na mpaka hivi sasa hali yake inaendelea vizuri lakini atakosekana kwa muda mpaka atakapopa nafuu na kuwa katika hali ya kawaida, 
 
kwa niaba ya O.F.A inamtakia kinda huyo afya njema na uvumilivu katika kipindi hichi kigumu kwa pande zote mbili upande wake na wa klabu,O.F.A ipo pamoja na nyota huyo kwa muda wote atakaokuwa nje na tunaomba wadau kumsaidia nyota huyo kwa hali yoyote wanayoona inafaa ili kujisikia kama taifa linamuhitajia sio tu akiwa mzima bali hata katika hali ngumu kama hio.
 
Chipukizi wa U17 wameendelea vizuri na michuano hiyo hiyo baada ya kuiramba F.C Porto bao 1-0 bao lilofungwa na Abdularazak Kheri ( De Jong) kwa shuti kali lililomshinda kipa wa F.C Porto na kujaa moja kwa moja wavuni na kuandika point tatu njingine kwa vijana hao wa U17.
 
Kwa matokeo ya mechi hizo za mwishoni mwa wiki U20 wamefikisha points 7 katika mechi tatu za awali ambapo wameshinda mbili na kutoka sare moja,
 
Nao ndugu zao wa U17 wametimiza points 10 katika mechi nne walizocheza kwa kushinda michezo mitatu na sare moja, tunawashukuru wadau wote waliojitokeza kwa namna moja au ningine ya kuwasapoti vijana hao na kuwaomba wadau wengine kujitokea kutoa ushirikiano wowote ambao wanaona unafaa katika kuandika sura mpya ya soka kwa vijana nchini kwa maendeleo ya ajira kwa vijana pamoja na maendeleo ya taifa letu.