UWEKAJI NYASI BANDIA YA UWANJA WA AMAAN

Kiwanja cha Amaan kikiwa katika hatua za mwisho mwisho wa matengenezo ya kuweka nyasi bandia kwaajili ya matumizi sio tu kwamashindano na sherehe za miaka 50 ya uhuru wa Zanzibar bali ni kiwanja ambacho kinatarajiwa kutumika katika mashindano mengine  makubwa kama ya vilabu vya afrika katika mashindano ya mabingwa ya Afrika na mashindano ya washindi wapili wa Afrika pamoja na yale ya Afrika mashiriki na kati pamoja na yale ya ligi kuu ya Zanzibar.
 
Kiwanja hicho kikiwa katika hatua ya kumalizika kwalengo la maendeleo ya soka sio tu kwa Zanzibar bali pia kwa Tanzania kwa ujumla kwa maendeleo ya Taifa katika nyanja mbalimbali kwa vijana wake/wananchi wake ambao wengi wao hutumia michezo kama ajira zao hasa ukiangalia vijana wengi  kila mwaka humaliza masomo yao na kukosa ajira hivyo kila mwaka serikali kuongeza idadi ya wananchi wasiokuwa na kazi hivyo michezo ndio njia kuu ya wananchi hao wadogo kujikomboa katika umasikini.
 
Wakati serikali ikiwekeza uwanja huo kwaajili ya "future" ya maendeleo ya soka pamoja na michezo mingine kama Riadha,nadhani maendeleo hayo wanahitajika hivi sasa kwa walengwa watakaokuja kutumia kiwanja hicho ambao ni vijana wadogo kwa kuweza kuwasaidia katika hali mbalimbali ili kuja kuwa ndio wakombazi wa maendeleo ambayo serikali imewekeza katika kiwanja hicho amabcho ni sawa na "kujenga mabanda ya kufuga kuku,huku ukijua hakuna mpango wowote hata siku moja wa kuja kufuga  kuku hao katika mabanda hayo", hapo nadhani itakuwa ni upotezaji wa wakati na uharibifu wa mali.
 
Tunatarajia kuwa wahusika wa mambo ya michezo mara baada ya kumalizika kwa sherehe za mapinduzi ya Zanzibar ya kutimiza miaka 50 wataweza kumurika "darumini"yao kwa vijana wadogo ambapo Zanzibar imebarikiwa kuwa katika moja ya nchi zenye vipaji na kuwa na mpango mzuri wa kuwaendeleza vijana hao wadogo ingawa kwa hali ngumu bila msaada wa taasisi husika lakini ni kuwa hao nyota wote wa zanzibar wanaochezea ndani na nje ya nchi wamekuwa wakiibuliwa kwa mpango huo katika ligi za Central League.
 
Huku Tanzania ikiwa waandaaji wa mashindano ya soka ya Afrika U17 mwaka 2019 Zanzibar ni moja ya wazalishaji vijana wenye vipaji vikubwa hivyo tunatarajia kuona Serikali inatoa ushirikiano mkubwa wa vijana wake ili kutoa vijana wengi iwezekanavyo kutokana na uwezo mkubwa wa vijana wake ambao pia walionyesha hivi karibuni baada ya kutwaa kombe la copa coca cola nchini.
 
Kwa upande mwingine hivi karibuni kulikuwa na kikao kati ya TFF na ZFA ambao ulikuwa ni mwanzo mzuri wa kufungua ukurasa mpya wa maendeleo ya soka nchini hivyo katika waliyozungumzia ni kuisaidia Zanzibar kupata ushiriki wake katika Fifa kama ambavyo nchi za Welles,Scotland,Nothern Irelands zinavyofanya pia mwanachama mpya wa Uefa Gibrolata wakiwa chini ya Spain watashiriki kwa mara ya kwanza mashindano yote ya Uefa hivyo mazungumzo hayo ya viongozi wa juu wa TFF na ZFA na mwanzo mzuri wa kufikia hatua kama mifano ya hapo juu inavyoonesha kwa hizo nchi. Wakati mipango hio ikiwa inatarajiwa kuanza kuchukua sura mpya hivyo kusubiri matokeo ya maongezi na ufuatiliaji wake hadi mwisho.
 
Katika mazungumzo hayo kulikuwa na mada ya kuona uwezekano wa kuirejesha ligi kuu ya Muungano/Tanzania ambayo ilikuwa na ushindani mkubwa miaka ya nyuma pia kupelekea timu nyingi kuwa na wafadhili kutokana na mashindano hayo yalikuwa na mashabiki wengi waliokuwa wakihudhuria katika mashindano hayo pamoja na mambo mengine mengi yaliyowavutia wawekezaji katika soka ukilinganisha na sasa.
 
Hakuna shaka Zanzibar ni nchi yenye wananchi wengi wanaopenda soka kama zilivyo nchi nyingine duniani,lakini tokea kupotea mfumo wa ligi ya Muungano ligi ya Zanzibar imepoteza muelekeo wake kwa pande zote, kutokana na kikao cha hivi karibuni cha viongozi hao sio siri kuwa Zanzibar na Bara wote wanahitajia ligi hio kwa lengo la kuibua wachezaji wa Taifa.
 
Tayari mfumo huo wa ligi umekubalika kwa pande zote mbili bila ya wenyewe kujijua na hivyo muhimu ni kuanza tu kwa mchakato wa kuanza ligi na aina yake kwa washindi wake,
katika kikao hicho ( ambacho kiliandaliwa na kampuni ya bia ya serengeti) tayari hapo viongozi wa ZFA walishiriki kikao ambacho kiliandaliwa na (kampuni ya bia,serengeti) hivyo katika kikao hicho aidha viongozi hao walikunywa (Maji na sio bia,maji ambayo yalinunuliwa kutokana na fedha za bia,au aidha kula chakula,au usafiri wao wa kwenda kikaoni au hata malipo ya hoteli ya kikao kilipofanyika ilikuwa ni malipo ya kampuni ya bia serengeti) hivyo tayari ZFA wamecheza na TFF katika mashindano/kikao kilichodhaminiwa na Bia Serengeti.
 
Muhimu ni kuwa hivi sasa ligi ya Zanzibar inadhaminiwa na Grand Malta, na ile ya bara inadhaminiwa na Serengeti, hivyo ligi hio ni rahisi sana kuicheza kama ligi ya muungano kwa upande wa bara kutumia wafadhili wao, na Zanzibar kutumia wafadhili wake, kama ambavyo Kmkm imecheza mechi za kirafiki na Simba/Yanga wao wakiwa na Serengeti katika mashati yao na kmkm wakiwa na Grand Malta, na wale wafadhili wa Vodafone wao wataingia mikataba ya ligi hio kwa pande zote mbili za Zanzibar na Bara na kama wafadhili wengine pia wataingia mikataba kwa pande zote mbili ili kuimarisha kipato cha pande zote. (kama bara wafadhili wao ni wa bia, visiwani watacheza wakiwa na wafadhili wa maziwa au maji katika mashati yao).
 
Mashindano ya Tusker Challenge Cup yamekuwa yakiandaliwa kwa miaka mingi na kampuni ya bia Tusker ya kenya ambapo Zanzibar imekuwa ikishiriki mfululizo mashindano hayo hata kama hawavai shati za udhamini huo lakini wanatumia "vitu vya wadhamini hao" nadhani mashindano mengi ya kimataifa unapocheza na timu pinzani kutoka nje inategemea udhamini wao huko kwao, inaweza kuwa ni wa "kamari au bia" lakini timu zetu zinacheza na vilabu hivyo katika mashindano ya ubingwa Afrika, sio kila timu ina matangazo ya coca cola tu tunazocheza nazo.
 
Nadhani mashindano ya ligi ya Muungano kila mmoja akitumia mdhamini wake,itakuwa ni kama mechi ya kmkm vs Yanga/simba na hakuna mabadiliko ambapo hakutakuwa na bango lolote la bia katika uwanja wa Amaan au Gombani na bara hakutakuwa na bango la Grand Malta. Lakini je bingwa atashirikia mashindano gani?
 
Nadhani ligi ya MLS inayo majibu yake kule Amerika kwani wanacheza ligi pamoja na Canada, lakini zote zinashiriki mashindano ya mabingwa wa South Amerika.
Mabingwa wa mashindano ya ligi ya Muungano kwa kila upande ataiwakilisha bara au visiwani kila upande kivyake katika mashindano ya ligi ya mabingwa na washindi wapili ili kunusuru timu za Tanzania kuendelea kuwa 4 katika mashindano hayo baada ya mbili kama majirani zetu pamoja na nchi nyingine nyingi za Afrika zilivyo hivi sasa. lengo ni kuboroshe ligi yetu kupata timu hizo 4 bora katika mashindano ya kimataifa na tusiwe kama washiriki tu wa mashindano hayo kila mwaka.
 
Mwisho aidha timu 4 bora kwa kila upande za msimamo wa mfumo wa ligi ya Muungano zitajigawa mara mbili 4 bara na 4 zanzibar ili kupiga fainali ya nguvu kila mmoja na upande wake wa kumpata bingwa wa upande wake na mshindi wa pili watakao wakilisha nchi hizo CAF. aidha ikiwezekana dhamana ya ligi kuu na mashindano ya CAF yanatosha kwa bingwa wa bara na zanzibar kujiandaa vizuri na mashindano hayo na kuiwachia nafasi ya kushiriki kombe la afrika mashariki na kati kushindaniwa kwa mtindo wa FA cup ambao utakuwa na sura muungano kwa timu zote za bara na visiwani kuanzia daraja la 3 ili kuweza kuliweka soka letu kuwa katika hali ya kisasa.
 
kwakuongezea tunatarajia uongozi wa wanaohusika na michezo Zanzibar wataweza kuutumia uwanja wa Amaan kwa lengo la kizazi kijacho kutayarishwa kuanzia sasa ili kuenda sambamba na uwekezaji wa uwanja huo na usiwa kama mapambo tu au gofu kama uwanja wa Mao tse tung ulivyo.