Uzinduzi wa majani Bandia Uwanja wa Amaan

Uwekaji wa majani bandia katika uwanja wa Amaan umekamilika kwa ufunguzi wa uwanja huo uliofanywa na Mh Waziri wa Afya Juma Duni Haji (pichani) nyuma yake ni mwenyeji wake Mh Said Ali Mbarouk waziri wa Michezo,Tunatarajia uwanja huo utaleta manufaa kwa vijana wadogo pia na kuondokana na sera za timu kubwa tu kuwa na haki ya kutumia uwanja huo na kufanya hata michuano ya fainali kwa timu za vijana kuchezwa katika viwanja vilivyochoka na kupunguza uwezo na mvuto wa michuano hio ya fainali ambazo kwa kawaida huzishirikisha timu bora za Zanzibar kwa wakati huo.

Tunatarajia uongozi wa michezo nchini utakuwa na sera mpya za kunufaisha vijana wake ambao ndio warithi wa uwanja huo muda mfupi ujao na pia kuwa ndio mwanzo wa kuziruhusu timu za Taifa za vijana za umri mbalimbali Zanzibar kuanza kufanya kazi sambamba na kiwango cha uwanja huo kilivyo sasa.