MALENGO YA KITUO CHA ORANGE FOOTBALL ACADEMY

Kituo cha OFA Orange Football Academy2014/2015

Kituo cha OFA kupitia timu zake za vijana za Orange zinazoshiriki ligi za Vijana kwa madaraja ya U-20, U-17 na U-14 kwa ligi za Central hapa Zanzibar kimejipanga zaidi kuhakikisha kinazalisha na kulea vijana hao kwa misingi bora ili kufikia malengo yake ya kuuza vipaji hivyo sehemu tofauti,na kuhakikisha kinawasaidia vijana hao kwa njia moja au nyengine kurahisisha kupata ajira kupitia michezo hasa mchezo huu wa mpira wa miguu kupitia kituo cha Orange football academy chenye makao makuu yake Zanzibar hapo Kikwajuni karibu na uwanja wa Mao ste tung chini ya Mwalimu wa kituo hicho Nd. Hashim Ali Kibabu.

 

Kituo kimeweza kufikia malengo makubwa kwa misimu miwili iliyopita 2012/2013 – 2013/2014, hata hivyo si kituo tu kilichofikia malengo hayo bali ni kwa vijana wote na wanamichezo kwa ujumla waliondani ya Wilaya ya Mjini Magharibi.

 

Mafanikio hayakuwa yakionekanwa kwa wachezaji tu bali hata kwa upande wa mwalimu (Kocha) wa kituo cha OFA kupitia timu za Orange Nd. Hashim Ali Kibabu ambapo yeye kwa upande wake aliiwezesha timu ya Orange F.A kufikia rikodi ya msimu uliomaliza 2012/2013 kukifikisha kituo katika nafasi ya pili ya kugombea Ubingwa, na msimu uliofuatia 2013/2014 timu ya Orange iliweza kufikia rikodi hio pia,

 

Kutwaa ubingwa ni jambo zuri sana hasa  kutokana na ubora wa vijana wetu, lakini lengu letu kuu ni sio Ubingwa tu bali ni kuhakikisha kila mwaka tunatoa vijana bora ambao wataweza kuchezea vilabu mbalimbali ndani na nje ya nchi.

Katika mafanikio yaliyochangiwa kwa kiasi kikubwa na kituo chetu cha Orange Football Academy ni pamoja na yale mafanikio ya kuiwezesha timu ya Kombaini ya Wilaya ya Mjini kutwaa Kombe la ubingwa wa Muungano kwa U-17 huku kituo chetu kikiongoza kwa kusheheni vijana watano tegemeo katikakikosi hicho cha mabingwa wa muungano.

 

Vijana hao nyota wa baadae wa taifa ni Abdulrahman Sulubu (Gerad), Adam Ali (Edo), Issa Omar (Mox), Abdulswamad Mussa (Walcot) na Mjaka Abdalla (Stopa) sambamba na mwalimu Hashim Kibabu ambae alikuwa kocha wa Kombaini hiyo na kuiwezesha kuipa Ubingwa msimu 2013/2014 kwa mashindnao ya Kombaini za Mawilaya.

 

Mbali na mafanikio hayo, kituo kimeweza kuzalisha vipaji vingi tu ambavyo msimu huu wa 2014/2015 vijana wa OFA wamekuwa wakitapakaa kila msimu katika  timu mbali mbali za madaraja ya Vijana Central Leage na zile za Tatu, Madaraja ya pili na lize za Ligi Kuu ya Zanzibar hivyo kivisaidia vilabu hivyo ambavyo havina timu za vijana kuendelea kukitegemea kituo chetu cha O.F.A pamoja na timu njingine nyingi zinazolea chipukizi kama hao.

Kituo chetu kipo kwa ajili ya kuzalisha, kulea na kuendeleza vipaji  pamoja n a kuhakikisha kinawatengezea njia za kuwapatia ajira kupitia kucheza mpira wa miguu ambao ni moja ya kazi kama kazi njingine yeyote duniani kote.

 

Pamoja na malengo hayo yote ya kituo chetu tunajikuta tukikabiliwa na changamoto kubwa katika vifaa na fedha za kuwahudumia vijana hao ambapo kituo chetu mpaka hivi sasa hakina mradi wowote au kitengo chochote cha kuweza kujipatia kipao cha kuwasaidia vijana hao ili sio tu kuwaondoa vijana hao katika vitendo vya kihuni bali pia kuwabunia njia ya kuwawezesha kupata ajira zao siku za mbeleni kutegemea mpira wa miguu na kuja kuliwakilisha taifa letu hapo baadae.

 

Kituo kwa sasa kipo katika maandalizi ya msimu wa 2014/2015 na ni moja katika changamoto kubwa ya kuhakikisha kinawaandaa vijana vizuri, ikiwemo kuanza harakati zake za kusaka vipaji kwa njia ya kuanzisha Bonanza la vijana, kusaka vipaji sehemu mbali mbali kutoka katika timu nyengine za vijana na kuwaweka katika kituo na kuwaendeleza na kuwalea kwa lengo la kuwaweka imara na kuwakuza viwango ili kuweza kujitangaza na kuonekanwa ndani na nje ya nchi kwa alengo la kuwapatia ajira ya kucheza mpira wa kulipwa.

 

Tayari hapo awali kituo kiliweza kuonyesha njia, kabla ya kupata mawazo ya kuwa kituo Rasmi, kiliweza kuzalisha vijana wengi na kutokomea timu mbali mbali za ndani na nje ya nchi. Kwa mfano hai OFA ilikuwa ni timu ya vijana ikitambulikana kwa jina la Flamingo na ikishiriki ligi za vijana, na iliweza kujitangaza kwa kuzalisha vipaji vingi kama 

Adam Nditi ambae atakipiga katika timu ya ( Cheasea Fc ya London),

Nassor Ali Nassor "kibichwa" ( New Castel United ya England)

Nassor Said " Cholo"  ( yupo katika timu moja ya ujerumani)

Seif Abdalla "Karihe" ( Azam Fc)

Mudathir Yahya "Muda" ( Azam fc),

Pamoja na wengine wengi wanaohezea katika timu za madaraja mbalimbali nchini.

 

Lakini pamoja na maendeleo hayo ni kuwa kituo chetu cha Orange Football Academy hakikupata hata senti tano ya mchezaji yoyote hivyo kukifanya kituo chetu kukabiliwa na changamoto kubwa ya fedha za kukiendesha kituo chetu kutokana na kutokuwa na faida yoyote ndani nchi au kutopewa thamani na wahusika kwa lengo la kuleta maendeleo ya nchi kupitia mradi huu uliobuniwa na vijana wenu.

 

 

Kupitia timu zake Orange Football Academy, timu za vijana U-20 bado kina ndoto njema za kuhakikisha kinazalisha akina Mesi, Ronaldo n.k na kuwasambaza duniani kote,

Tunawaomba wahusika wa michezo na wadau wapenda maendeleo wote nchini kujitokeza kukisaidia kituo chetu,hasa ukitilia maanani kuwa tayari kituo kinaana kutushinda kukihudumia na hata tunatarajia msimu huu kubakia na timu moja ya U20 kutokana na kutoweza tena kugharamia vijana wengine wa U14 ambao hawa ndio muhimu zaidi katika misingi ya maendeleo nchini.