MATOKEO YA MECHI ZA FAINALI KWA MADARAJA YA VIJANA CENTRAL LEAGUE WILAYA YA MJINI - 2013/2014

 

KOMBE LA LIGI DARAJA LA JUVENILE

Bingwa Azam Zanzibar  mshindi wa pili real kids

Kombe la mtoano Juvenile

Bingwa zafsa   mshindi wa pili Azam Zanzibar

mechi ilitoka sare dakika 90* penaltiZafsa 5 Azam znz 4

 

KOMBE LA LIGI DARAJA LA JUNIOR

Bingwa New Star Soccer  mshindi wa pili Nyaru Kids

Kombe la mtoano Junior

Bingwa F.C Royal   mshindi wa pili Orange F. Academy

mechi ilitoka sare dakika 90* penaltiRoyal 4  Orange 3

 

KOMBE LA LIGI DARAJA LA CENTRAL

Bingwa Villa S.C mshindi wa pili amefutwa kwenye mashindano kutokana na utovu wa nidhamu Kombe la Mtoano Central  

 

PAMOJA NA KUKABIDHIWA ZAWADI KWA WASHINDI NA

KUFUNGA MSIMU 2013/2014

Zawadi mbali mbali zilitolewa na kukabidhiwa kwa Mshindi wa kwanza na wa Pili kwa mashindano ya ligi na ya mtoano.

kwa madaraja yote matatu: Central, Junior na Juvenile.

Pia zawadi mbali mbali zilitolewa kwa wachezaji, bora (Man of the Match) - “Ishak K. Nassor, Omar Ame na Ibrahim Makungu na mchezaji mwenye kipaji maalum ni Mahmoud Ali – Miaka 12.

Zawadi pia zilotolewa kwa upande wa vyombo vya habari, na mwandishi wa habari bora alipatiwa zawadi (Nd. Abubakar Kisandu) kutoka Coconut FM Radio. 

 

MSIMU WA LIGI UMEMALIZA 2013/2014

 

HUKU TUKITEGEMEA MAKUBWA KUTOKA KWA KITUO CHA “OFA” ORANGE FOOTBALL ACADEMY ambacho ni kituo cha kukuza na kuendeleza vipaji kwa Vijana hapa Zanzibar. Timu hiyo ya Orange licha ya kufanya vizuri 2012/2013 Mshindi wa Pili Ligi ya Junior na 2013/2014 Mshindi wa Pili ligi ya Mtoano Junior.  Chini ya Kocha Hashim Ali Kibabu ambae kocha huyo wa Orange kwa misimu hiyo miwili Amepata mafanikio makubwa (Mshindi wa Pili ligi Junior 2012/2013, Ubingwa kombaini za Wilaya Sherehe za Muungano Cup 2013/2014 na Mshindi wa Pili wa Kombe la Mtoano Junior 2013/2014. (Kamati haijamuona na kumpa hata tunzo moja!) huku tukiona tunzo na zawadi mbali mbali wakipewa baadhi ya wachezaji, timu bingwa, waandishi na vyombo vya habari.

 

Kuna usemi usemao: “mcheza kwao hutunzwa” kocha Hashim kibabu amefanya kazi kubwa katika kuipatia sifa na kuitangaza wilaya ya mjini katika soka la vijana kupitia timu ya kombaini ya wilaya ya mjini, kituo cha “ofa” ambacho kipo wilaya ya mjini na kupitia timu ya Orange Football Academy ambayo anafundisha na kuipa mafanikio.

 

Ama kweli sahau ni ibada: muda upo, tulipo kumbuka wakati huo tuutumie kufuta makosa yetu ya kusahau, na kutekeleza wajibu wetu. Nadhani, mwenye kufanya vizuri anahitaji kupongezwa.

 

Tujenge ngome nzuri ya kuwaenzi watu kama hawa katika michezo tukiwakosa, na wakitutoroka hatutofika mbali. Hashim kibabu ni mdau, mwanamichezo, kiongozi, mchezaji, kocha, mtoa ushauri na pia anasaidia kazi kubwa na ngumu katika ufuatiliaji na utangazaji wa habari za michezo.

                                                       

 

Kituo cha Orange (OFA) 2013/2014 kimejivunia matund aambayo kipepanda moja wapo ni kuweza kutoa wachezaji wengi katika timu za Kombaini kwa ngazi ya U-20 na U-17 na Kocha wa Kituo hicho Hashim Ali Kibabu alikuwa kocha wa Kombaini ya U-17 ambayo ilishiriki ligi za Muungazo kwa Wilaya za Unguja na timu hiyo kufanikisha kuchukua Ubingwa wa Kishindo, katika michezo yake yote iliyocheza timu hiyo iliweza kushinda magoli mengo, nusu fainali ilishinda 5-0 kwa kuifunga Kusini na fainali ilishinda 6-0 Kuifunga Magharibi na kuweza kutwa Ubingwa huo Wilaya ya Mjini kwa mara ya Kwanza na kwa kishindo chini ya Kocha Hashim Ali Kibabu ambae ni kiungo muhimu katika kulea kukuza na kuendeleza vipaji kwa vijana hasa katika kituo cha Orange (OFA) hapa Zanzibar.