Picha Za Na Matukio Ya Ufunguzi Wa O.F.A Website

Pichani ni baadhi ya viongozi mbalimbali wa soka nchini waliohudhuria katika uzinduzi wa orange football academy offical website wiki iliyopita.
 
viongozi mbambali,waandishi wa habari,makocha,wachezaji na wadau wa soka  walihudhuria katika uzinduzi huo ambapo kituo cha kukuza soka kwa vijana nchini ORANJE FOOTBALL ACADEMY kikiendelea katika mikakati yake ya kuchangia soka kukua nchini.
 
Mbali na soka  pia kuwaweka vijana kuwa na misingi mizuri ya kujipatia ajira siku zijazo kupitia soka ,afya njema kupitia soka pamoja na kuwalea na  kuwajenga vijana kuwa na mafunzo mazuri na kujiepusha na vitendo vinavyokatazwa katika jamii.

Tunawaomba wadao wote nchini kukisaidia kituo chetu cha kukuza vipaji  nchini ORANGE FOOTBALL ACADEMY kwa mchango wowote ambao kila mdau ataona kuwa unafaa kuwasaidia vijana wetu ili kufikia malengo na kulifanya taifa letu kunufaika  na pia kuwasaidia vijana hawa wadogo ambao ndio taifa letu la kesho.

tunawaomba wadau wote kutumia website hii kutangaza biashara zao ili kituo chetu kiweza kujipatia uwezo kidogo wa kuwaendeleza vijana hawa wadogo  ambao kituo chetu mpaka sasa kinaendea huku kikiwa na upungufu mkubwa wa vifaa ,madawa,mipira  na mengineyo.
 
tunawaomba wadau wote nchini kwa  wenye kutaka kushirikia na kituo chetu tunawakaribisha kuungana na kituo chetu ili kwa pamoja tuweza kuwasaidia vijana wetu na kilisadia taifa letu kufikia katika malengo ya kulikomboa soka nchini kama ambavyo serikali imeweka mikakati hio mipya ya soka la yosso ili taifa letu liwe kama mataifa mengine duniani.