Sherehe Za Kukabidhi Vyeti Olympafrica Tanzania (Toc)

Katibu mkuu wa Kituo cha kukuza soka kwa vijana nchini cha ORANGE FOOTBALL ACADEMY ngd Hussein alihudhuria  katika sherehe za kukabidhi vyeti kwa wahitimu wa mafunzo ya Futbalnet akiwa ni katibu wa kituo hicho pia ni mgeni mwalikwa kutokana na nafasi yake ya kuwa  katibu wa Central League wilaya ya mjini na pia ni katibu mkuu wa O F A na ni mtu ambae yupo mstari wa mbele katika kuhamasisha utafutaji na uendelezwaji wa vipaji vya vijana nchini. 

 
 
Suleiman Mahmoud Jabir ( Teacher Sule )Mjumbe wa kamati ya T O C na Mwenyekiti wa kamati ya ufundi ya T O C ambae pia ni Mkurugenzi wa Ufundi wa Z F A  akikabidhi vyeti kwa wahitimu wa mafunzo ya Futbalnet Hafla iliyofanyika hivi karibuni huko Dole wilaya ya Magharibi Zanzibar katika kituo cha OlympAfrika Tanzania kilichopo huko Dole. Mchezo wa Futbalnet ni mchezo wa mpira wa miguu unachezwa kwa kuzingatia na kuheshimu makubaliano ya timu mbili zinazocheza.
 
 
 Washiriki wa mafunzo ya Futbalnet ambao wengi wao ni walimu wa skuli
 

 

Wachezaji wa timu mbili  wakikubaliana taratibu na sheria wanazohitaji kuzitumia kwenye mechi yao kabla ya kuanza kwa mchezo husika kama zilivyo ama zinavyotaka taratibu za futbalnet na walimu wao wakishuhudia na kuandika makubaliano hayo kabla ya kuanza kwa mechi

 
Timu kepteni wa kituo cha Olympafrika Zanzibar akinyanyua juu kikombe cha ubingwa mara baada ya kukabidhiwa na mgeni rasmi Bi Nasra Juma mjumbe wa kamati ya T O C . Tanzania Olympic Committee.
 
Katibu mkuu wa Kituo cha kukuza soka kwa vijana nchini ngd Hussein alihudhuria  katika sherehe hizo akiwa ni katibu wa kituo hicho pia ni mgeni mwalikwa kutokana na nafasi yake ya kuwa  katibu wa Central League wilaya ya mjini na pia ni katibu mkuu wa O F A na ni mtu ambae yupo mstari wa mbele katika kuhamasisha utafutaji na uendelezwaji wa vipaji vya vijana nchini.