NYOTA WANNE WA O.F.A U17 WAITWA KATIKA KIKOSI CHA WILAYA YA MJINI

Vijana wa Kituo cha OFA orange football Academy  jana Jumapili tarehe 01/12/2013 timu zake za Vijana Centra U20 na Junior U17 zilicheza mechi za ligi iliyoanza hivi karibuni,
matokeo U20 OFA  1-1 KWAHANI 
U17 OFA  2-0  MAPEMBEANI, 
goli la OFA kwa U20 limefungwa na Fahad Adam (Alaves) kwa mkwaju wa frikik,  na magoli ya U17 yamefungwa na Jaffar Ussi (Jefu) kwa goli ambalo huenda likawa la msimu alilolifunga kwa njia ya  tiktaka dakika ya 37 na lile la pili limefungwa na Adam Ali Issa (Edo) ambae amefikisha magoli matatu kwa mechi tatu. kila mechi anafunga goli moja.
 
hata hiyo OFA U20 yasikitishwa na matokeo mabaya na kutokuhudhuria mazoezi kwa wachezaji wake kama inavyohitajika kuwajengea vizuri zaidi uwezo wao kutokana na umri wao huo kuhitajika zaidi katika soka.
 
Hata hivyo kiungo mchezeshaji Abdulhalim (Kizizu) ameanza kwa mara ya kwanza kucheza mechi ya ligi baada ya kukosekana kwa muda mrefu, pia ameonyesha kiwango kizuri na cha kuvutia.

Wakati huohuo Kocha Hashim Ali Kibabu ameteuliwa kuwa mmoja ya makocha wawili wa timu ya Wilaya ya Mjini Magharib U17 na hivyo emepewa kazi ya kuchagua kikosi cha Kombain ya Wilaya hiyo yenye sifa ya kuwa na nyota wengi wa soka  kwa umri mbalimbali.
Katika uteuzi huo ambao ameanza mara moja kazi hiyo kwa lengo la kuimarisha vipaji vya soka  kwa vijana wa umri mbalimbali hivyo kupewa  jukumu hilo la kuifundisha timu ya U17 katika uteuzi huo kutoka Kamati ya Central League Wilaya ya Mjini Magharib,
 
Chipukizi wanne kutoka katika kituo cha OFA wamepata nafasi ya kuwemo katika kikosi cha Kombain ya U17 baada ya kuonyesha uwezo mkubwa na nyota ambao kocha kutoka nchini Ufaransa Patrick Liewig alisema wachezaji hao watunzwe vizuri kwani wana uwezo mkubwa sana kisoka.
 
Nyota hao ni Kepteni wa U17 Abdulrahma Shaaban (Gerad), Adam Ali Issa (Edo), Issa Omar (Mox, Kipa) na Abdulsamad Mussa (Walcot) kocha Hashim Ali Kibabu atashirikiana na Moh'd Salahi (Edi salahi) katika kukinoa kikosi hicho ambacho kitasheheni njota kutoka katika timumbali za wilaya ya mjini Magharibi.
 
Kwaniaba ya Kituo cha O.F.A kinatoa pongezi kwa nyota wake wote walioteuliwa katika kikosi hicho pia kutoa pongezi kwa mwalimu wake Hashim Ahmada kwa kuteuliwa kwake kuwa mmoja wa makocha wa kikosi hicho.
 

Tunawaomba wadau na wafadhili wa soka nchini kujitokeza kuisaidia timu hio ambayo ndio hazina kubwa kwa taifa hapo baadae ambao baada ya serikali kuwekeza katika kutengeneza kiwanja cha Amaan na baadae mao tse tung kuwa hawa ndio wachezaji na wawakilishi wa nchi katika mradi huo wa ujenzi wa uwanja unaoendelea kutandikwa nyasi za bandia hivi sasa.